IMAM HUSAYN IBN ‘ALI A.S Bwana wa mashahid

 

 • Jina: Husain ibn Ali
 • Jina la kupewa: Sayyid-as-Shuhadaa (kiongozi wa mashujaa)
 • Kuniya: Abu Abdullah
 • Kuzaliwa: Alhamis, 3 Shaban Mwaka wa 4 Hijiria. Katika mji wa Madina.
 • Baba: Imam Ali bin Abi Talib (Amani ya Mwenyeezi Mungu iwe juu yake),
 • Mama: Bibi Fatimah (Binti wa Mtume s.a.w.w)
 • Kufariki: (ameuwawa akiwa shahidi) siku ya Ijumaa, 10 Muharram, mwaka wa 61 Hijiria.
 • Sehemu alozikwa: Karbala, Iraq       akiwa na umri wa miaka 57.

Amezaliwa Imam Husein – Amani ya Mwenyeezi Mungu iwe juu yake, usiku wa Alhamis tarehe 3 mwaka wa 4 Hijiria mwezi wa Shabaan katika mji Mtukufu wa Madina.

Baba yake alikuwa ni Imam Ali Bin Abi Talib – Amani ya Mwenyeezi Mungu iwe juu yake, aliyekuwa mfano bora, kwa utukufu na uchamungu baada ya Mtume s.a.w.w, kwa wema mbele ya marafiki zake na shujaa dhidi ya maadui wa Uislam.

Na mama yake alikuwa ni  Fatimah, binti na mtoto peke wa Mtukufu Mtume s.a.w.w, aliyepata kuwa mwanamke bora  ulimwenguni aliyerithi sifa, elimu na maarifa kutoka kwa  baba  na mama yake Bibi Khadija Bint Khuwailid.

Imam Husein  ni wa 3 katika  Maimamu 12 waliotoka katika nyumba tukufu ya Mtume s.a.w.w.

Wakati habari njema ya kuzaliwa kwake kufikiwa kwa  Mtukufu Mtume, akaenda nyumbani kwa binti yake, akamchukua mtoto na kumweka katika mikono yake, kisha akasoma Adhana katika sikiolake la kulia na Iqamah katika sikio la  kushoto, na  baada ya siku 7 ya kuzaliwa kwake, alifanya ibada ya aqiqah , na kumpa jina la al- Husayn, kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu .

Abdullah ibn Abbas anasema:

“Katika siku ambayo alizaliwa Imam Husayn a.s Mwenyezi Mungu alimuamuru malaika Jibril kushuka kwa ajili ya  kumpongeza Mtukufu Mtume s.a.w.w . Wakati wa kushuka  Jibril alipita juu ya kisiwa ambapo malaika aitwaye Futrus aliyekuwa amefungiwa hapo kutokana na kuchelewa kwake katika kutekeleza yale aliyoagizwa na  Mwenyezi Mungu. Hivyo alikuwa amenyimwa mbawa na kukaa  kisiwani hapo  kwa miaka kadhaa akiomba na kumwabudu Mwenyezi Mungu s.w.t na kuomba msamaha wake. ”

Pindi malaika Futrus alipomwona Jibril, alimwita na kumuuliza: “unakwenda wapi, Ewe Jibril?

Naye akamjibu: “Husayn, mjukuu wa Muhammad amezaliwa, na kwa sababu hii Mwenyezi Mungu ameniagiza niende nikatoe pongezi kwa Mtume wake”,

Malaika Futrus akamwambia: “Je, unaweza kunichukuwa pamoja na wewe huenda  Muhammad akapendekeza kesi yangu kwa Mwenyezi Mungu?”

Jibril alimchukua malaika Futrus pamoja naye, hadi  kwa Mtume s.a.w.w, wakatoa pongezi kwa niaba ya Mwenyezi Mungu na kisha akawasilisha kesi ya malaika Futrus kwake.

Mtukufu Mtume s.a.w.w akasema kumwambia  Jibril, mwambie malaika Futrus agusa mwili wa mtoto aliyezaliwa ili aweze kurudi katika nafasi yake Mbinguni.  alipofanya hivyo tu malaika Futrus alirejeshewa  mbawa zake papo hapo na kumsifu Mtume na mjukuu wake aliyezaliwa, akapaa kuelekea Mbinguni.

Hasan na Husayn ni  wana wawili wa Imamu Ali ibn Abi Talib na Fatimah, mwanamke mwenye Nuru walioheshimiwa kama:  “Viongozi wa Vijana wa peponi” kama ilivyoelezwa na Mtukufu Mtume.

ImamHusayn  a.s aliuokoaUislamu.

Kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Mtume s.a.w.w ya kwamba:

“Husayn anatokananaMimina MimininatokananaHusayn”

inamaanakuwaImamHusayn a.s nisehemuyaMtumes.a.w.w. naharakatizaMtumes.a.w.w zimehuishwanaImamHusayn a.s. HililinatokananabarakazilizoambatananashahadayaImamHusayn kwaniilivuruganjamazakiovuzaMuawiyanamwanayeYazidizenyemalengoyakupambananaBaniHashimnahatakuufutiliambaliUislamunakuanzishataifalakiarabumahalipaUislamu.

muaissiwamapinduziyaKiislam ImamKhomeinir.a alisema:

“MaasiyaAshuranimfanoadhimukwawatuhuru. MtukufuImamHusseinia.s, BwanawaMashahidi, kwakitendochakealitufundishasisisotenamnayakusimamadhidiyaukatili, dhidiyaserikaliyaKidhalimu. Tangumwanzoalitambuakuwanjiaaliyopitailikuwaninjiaambayowafuasiwakewotenafamiliayakewangetolewamuhanga. Lakinipiaaliutambuamwishonamatokeoyake. Zaidiyahapoalitufundishakuwakatikahistoriayotehiindiyoitakuwanjiayakufuatwa; nakwambauchachewawatuisiwesababuyahofu. Sioidadibalinisifayawatundiyoinayofaa, vilevilesifayajihadiyawatudhidiyaaduindiyoinayohitajika. Idadiinawezakuwakubwalakiniikawanakasoroaukutofaa.

Vilevileidadiyawatuinawezakuwandogobadoikawamadhubutinayenyemafanikiokutokananasifayaoyajuu. ImamuhuyowaUislamualitufundishakusimamapindidhalimuanapowatawalawaislamukwaukatilihatakamanguvuzetunindogo. NaiwapoheshimayaUislamuikohatarini, tunatakiwakuyatoamaishayetukatikakuutetea”.

Bwanawamashahida.salionakuwaaidolojiayakiislamuilikuwaimeharibiwa.KusimamakwaImamuHusseini  a.saumapambanoyakiongoziwawaumini ,ImamAlia.sdhidiyaMuawiyahnakampenizaMitume  dhidiyamadhalimuna  wapaganiwakubwasiosualalakutwaaardhi

ImamuHusaynna.shakusimama  kumpingaYazidikwaniatuyakuutwaaufalmewaYazid, inaelezwakuwaImamu  a.salilitambuahilo, lakinihatahivyoalisimamaakitambuakuwaalitakiwakupambanadhidiyautawaladhalimu, nawakikatilihatakamaatalazimikakuyatoamaishayakenamaishayafamiliapamojananduguzake.

AdhuhuriyasikuyaAshurawakatimapambanoyakiendeleanawotewakiwahatarini,mmojakatikawafuasiwakealitoataarifakuwailikuwaniwakatiwasalayaadhuhuri. ImamHusayn a.s alisema:

 “umenikumbushajuuyasala. Allahakuhesabukamamtekelezajiwasala”

Kishaakasimamanakusalihakusematuendeleenamapambanohapana,kwasababumapiganohayoyalikusudiakuilindasala.

KamaisingekuwaAshuranamuhangawakizazichaMtumes.a.w, basidhalimuwazamahizoangeharibulengolamahubirinajuhudizaMtumes.a.w. KamaisingekuwaAshura, tusingeijuaQurannaUislamukwaujumla.

BwanawamashahidialisimamakuuimarishaUislamu,  kupingadhulmanakupambanadhidiyautawalawawakatihuoambaoulikuwaumepataupeowatawalazazamazasasa. Katikakufanyahivyoaliwatoamuhangawatotowakewadogo, wafuasiwakenahatimayemaishanadamuyakemwenyewehakuwanavituvyakiduniailiapatekuvitoa.

BwanawaMashahid (a.s) , nayepiaaliuwawahakufanyahivyoilikulipwa. Maliponisualaambalohalikuwananafasikwake. Alikwendakatikahaliyakuinusuruitikadi, kuuendelezaakuuhuishaUislamu.

ImamHusseina.s  aliuwawa  lakinihilolilikuwakatikakutiiamriyaMwenyeziMungu;ilikuwanikwaajiliyaMwenyeziMungu; Ilikuwaniheshimanahadhiyakenahivyo,hakushindwa bali  alitiiamriyaMwenyeziMungu.

‘Amani iwe juu yake siku alozaliwa , aliyoaga dunia na siku atakayofufuliwa”

Ameen

 

 

 

Advertisements

FADHILA NA A’AMALI ZA MWEZI WA RAJAB

 

Mwezi wa mtukufu wa Sha’aban na mwezi mtukufu wa Ramadhan ni katika miezi mitukufu. Zipo riwaya nyingi zinazoelezea ubora wa miezi hii. Imepokewa riwaya kutoka kwa Mtume wa Allah s.a.w.w isemayo ya kwamba:

 “Mwezi wa Rajab ni mwezi mkubwa wa Allah, ni mwezi wa Rehma na Fadhila, kupigana vita katika mwezi huu ni haram. Rajab ni mwezi wa Allah, Sha’aban ni mwezi wangu na Ramadhani ni mwezi wa Umma wangu”.

Yeyote atakayefunga japo siku moja katika mwezi wa Rajab atakuwa na furaha mbele ya Allah s.w.t. na ghadhabu za Allah zitakuwa mbali naye na mlango katika milango ya Jahannam (moto) itafungwa kwa ajili yake.

Imaam Musa bin Ja’afar a.s. amesema ya kwamba:

“Yeyote atakayefunga siku moja katika mwezi wa Rajab atakuwa mbali na moto wa Jahannam. Atakayefunga siku mbili katika mwezi huu kuingia peponi kutakuwa ni wajib kwake”

Na pia amesema:

“Rajab ni jina la mto wa peponi, maji yake ni meupe kuliko maziwa, utamu wake unazidi ule wa asali, yeyote atakayefunga siku moja katika mwezi huu basi atakunywa maji kutoka katika mto huu”

 

Na kutoka kwa Imaam Ja’afar Swaadiq a.s. amesema Mtume s.a.w.w amesema kwamba:

“ Mwezi wa Rajab ni mwezi wa toba kwa ajili ya Umma wangu, hivyo tubieni (ombeni msamaha) katika mwezi huu, kwa hakika Allah ni mwingi wa kusamehe na mkarimu, semeni kwa wingi:

استغفراللهواسالهالتوب

A’AMAL ZA MWEZI WA RAJAB

A’amal za mwezi wa Rajab zimegawanyika katika sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza

A’amal zinazohusiana na mwezi mzima, maalum kwa ajili ya mwezi wa Rajab isiyo na siku iliyoainishwa, nayo ni:

Kusoma du’a hii iliyopokelewa kutoka kwa Imaam Zainul Abidiin a.s. kwa mwezi mzima. Du’a hiyo ni:

یا من یملک حوائج السائلین و یعلم ضمیر الصامتین لکل مسئلت منک سمع حاضر و جواب عتید الهم و مواغیدک الصادقة و ایادیک الفاضلة و رحمتک الواسعة فاسئلک ان تصلی علی محمد و ال محمد و ان تقضی حوائجی للدنیا و الأخرة انک غلی کل شيء قدیر

 

Sehemu ya Pili

A’amal maalum za mchana na usiku katika mwezi wa Rajab

Usiku wa kwanza katika mwezi wa Rajab ni mtukufu mno, na katika usiku huu kuna A’amal hizi za kufanya:-

 1. kwa kuwa umeshauona mwezi unatakiwa useme:

الهم اهلّهُ علینا بالامن و الایمان و السلامة و الاسلام ربّی و ربّک اللهُ عزّ و جلّ

Pia imepokewa kutoka kwa Mtume s.a.w.w ya kuwa: “Kwa kuwa umeuona mwezi wa Rajab, sema:

الهم بارک لنا فی رجب و شعبان و بلّغنا شهر رمضان واعنّا علی الصیام و القیام و حِفظِ السان و غضِ البصر و لا تجغل حظّنا منه الجوع و الغطش

 

 1. kujitwaharisha kwa kufanya ghusl. Baadhi ya maulamaa wanasema: imepokewa kutoka kwa Mtume s.a.w.w ya kwamba:

“Yeyote atakayefikiwa na mwezi wa Rajab na akajitwaharisha kwa kufanya Ghusl mwanzo, katikati na mwisho wa mwezi wa Rajab, atasamehewa dhambi zake zote na kuwa kama alivyozaliwa kutoka katika tumbo la mama yake.”

 1. kumzuru Imam Husein a.s.

 

A’AMAL UMME DAWOOD

Hii ni ‘amal inayofanyika mchana wa siku ya  15 katika mwezi wa Rajab, kwa ajili kukidhi haja na kujiondosha katika balaa na matatizo mbalimbali.

Ni mustahab (sunna) kufunga siku hii hasa ukiwa na nia ya kuifanya A’amal hii, ikifuatiwa na haya yafuatayo:

 1. kujitwaharisha kwa kufanya ghusl (kuoga) kabla ya kuingia Adhuhuri.
 2. swali swala ya Adhuhuri na Alasiri
 3. kaa sehemu tulivu na uelekee Qibla na usijishughulishe na jambo lolote isipokuwa Dua, na soma:
 • suratu-fatiha x100
 • suratul-Ikhlaswix100
 • ayatul kursiyy x 10
 • suuratul An’am, bani Israil, kahf,luqman.yasin,swafaat, Hamim sajidah, Dukhaan, Fat-hi, waqi’a, mulk, nun,shaqat mpaka mwisho wa Qur’an
 • maliza kwa kusoma Dua ya Umme Dawood.

 

 

 

 

 

MAADHIMISHO YA MAZAZI YA BINTI WA MTUME WA UISLAM

Sherehe za mazazi ya mbora wa viumbe na mtoto wa mtume wa uislamu Bibi fatima a.s imefanyika leo katika ukumbi wa Masjid Al-hadeer Kigogo Post Dar es salaam Tanzania ikisimamiwa na umoja wa wanawake chini ya uongozi wa Zahra Foundation na ushiriki wa Hawzatul-imam Swadiq a.s.

IMG-20140426-WA0004 IMG-20140426-WA0006 IMG-20140426-WA0014zahraf

Maombolezo ya Msiba wa Bibi Fatima a.s

 

 

image1 (3) image1 (4)

Waumini wa kiislamu wamekusanyika leo sehemu mbalimbali kumkumbuka na kuomboleza kifo cha Bibi mtukufu Fatima a.s

Samahat Sheikh Hemed jalala Mudeer wa Hawzatuk-imam Swadiq a.s na imam wa sala ya Ijumaa katika msikiti wa Ghadeer kigogo Post jijini Dar es salaam ameungana na maelfu ya maulamaa kukusanya waumini ili kuwazungumzia tukio hili lenye kuumiza mioyo ya wanaompenda mtukufu mtume na kizazi chake.

Tunatoa salamu za rambirambi kwa Imam wa zama zetu Imam Alhujjatul-Muntadhar a.j na Kwa Sayyid Alqaid  Ayyatollah Al-marji Al-udhma Sayyid Ali Khamenei (d.d) na Marajii wetu na waumini wote kwa ujumla juu ya msiba huu adhim wa Bibi Fatima a.s
INNALILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUN WALAANATULLAH ALA DHWALIMEEN.

 

forBlog

Kumbukumbu ya Kifo cha Bibi Fatima a.s

Kulingana na kalenda ya historia ya waislamu na uislamu katika mwezi na siku kama ya leo Tarehe 3 jamadil-Akhir  mwaka 11 H   ni siku aliyoaga dunia mwanamke bora miongoni mwa wanawake wote tangu Dunia kuumbwa, kiliondoka duniani kioo cha kiwiliwili ambacho kila mtu duniani akijitazama kupitia kioo hicho lazima daima atabaki msafi na atatakasika kikwelikweli.

Bibi Fatima ni bint wa pekee aliyeishi katika mabinti wa bwana mtume s.a.w.w, ni mtoto wa mwanake bora miongoni mwa wale wanawake bora wanne waliochaguliwa na Allah.

Bibi huyu mbora aliweza kutumia sehemu finyu ya nyumba yake kumfundisha binadamu na hasa mwanamke vitu ambavyo upana wake ni zaidi ya upana wa Dunia, Alikua ni binti mdogo aliyeweza kubeba majukumu ambayo hayakuwahi kushuhudiwa na jicho lolote kabla yake, alimlea Baba yake mtukufu  mtume  wa Allah kwa mapenzi ambayo mtoto huwa anayapata kutoka kwa  mama, aliweza kumpa mtume s.a.w.w. zile hisia zote ambazo alizikosa kwa kufiwa na mama yake akiwa mchanga  mpaka mtume ikafikia kusema ” Fatima ni mama ya baba yake.“.

Bibi Fatima a.s aliozeshwa na Allah kwa Ali bin Abi Talib a.s ambae ni  mwanaume Bora kuliko viumbe vyote baada ya Mtukufu mtume s.a.w, ambae mtume s.a.w.w anamwambia Ali” Ewe Ali hakuna anaemjua Allah zaidi ya mimi na wewe na hakuna anaekujua zaidi ya Allah na mimi“.

Bibi Huyu alizawadiwa watoto ambao Quraan inambashiria mtume kuwa hao ndio watakaoendeleza kizazi kitukufu cha nyumba ya utume pale Allah alipomwambia mtume “hakika adui yako ndiye aliyekatikiwa na kizazi” suratul-kawthar, Allah anamwambia haya mtume kwa kuwa “INNAA A’TWAINAKAL-KAWTHAR“(hakika tumekupa kheri nyingi), Hii kheri nyingi hapa ni Bibi Fatima a.s,fatima3

Bibi Fatima aliuawa na wale walioshika madaraka baada ya Mtume s.a.w.w na alizikwa usikua bila watu kujua ila alisema yafuatayo katika maneno yake ya mwisho akimwambia Imam Ali a.s:

“Oooh Ali, unajua fika kuwa leo ni siku ya mwisho ya maisha yangu, Ninafuraha na pia ninahuzuni, ninafuraha  kuwa matatizo na machungu yangu yatakwisha na nitakutana na baba yangu, lakini ninahuzuni kwa kutengana na wewe.

Ali naomba uandike haya ninayokwambia na ufanye kama ninavyousia,”Baada yangu unaweza kuoa mwanamke yeyote yule utakaempenda lakini lazima umuoe binamu yangu Yamamma kwani anawapenda sana watoto zangu na Hussein moyo wake umefungamana nae sana, Muache Fidhwa aendelee kuishi na wewe hata baada ya kuolewa kwake kwani nilikua nikimpenda zaidi kama binti yangu.Ali NAOMBA UNIZIKE USIKU NA WALE WALIOFANYA UKATILI JUU YANGU WASIHUDHURIE MAZISHI YANGU…..“”

Sayyida Fatima aliusia maneno hayo hapo juu na Imam Ali alifanya kama alivyousiwa na alizikwa na watu wachache na kusababisha kaburi lake lisijulikane mpaka leo wakati imam Ali anamzika Hurul-aini huyu wa kibinadamu alisikika akisema”Ewe mtume wa Allah leo ninakurudishia ile amana yako“.

Mtume wa Allah anasema “Fatima ni pande la nyama katika sehemu ya mwili wangu, atakaemridhisha ameniridhisha mimi na atakaemuudhi ameniudhi mimi”.

HAIKUPITA MUDA MREFU TANGU KUONDOKA KWA MTUME DUNIAN WALIMUUDHI UMMU ABIHA, WAKAMNYANG’ANYA URITHI WAKE BALI PIA WAKAIVUNJA HESHIMA YAKE NA WAKAMPIGA NA KUICHOMA NYUMBA YAKE NA  KUPELEKEA KUKASIRIKA BINT YA MTUME MPAKA AKAUSIA AZIKWE USIKU.

Inna lilah wainnailayhi raajiun.

 

 

SAYYID SHUHADAA CHARITABLE COMMITTEE

Implementing The Teachings Of Ahlalbayt a.s

zahraa Foundation

Fatima bint Muhammad is the Symbolization of Women's Power in Islam

The Daily Post

The Art and Craft of Blogging

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.